Jumapili 1 Februari 2026 - 23:00
“Mpango wa Amani wa Ghaza ni usaliti dhidi ya Palestina na Umma wa Kiislamu”

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Baqir al-Husayni, Rais wa Jumuiya ya Imamiya ya Baltistan nchini Pakistan, katika hotuba yake aliuelezea mpango unaoitwa “Mpango wa Amani wa Ghaza” kuwa ni kinyume na maslahi ya Waislamu na ukiwa katika mgongano wa wazi na azma na muqawama wa Palestina. Alisisitiza kuwa amani ya kweli inaweza kupatikana tu pale ukaliaji utakapokoma na Palestina itakapokombolewa kikamilifu.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Baqir al-Husayni, Rais wa Jumuiya ya Imamiya Baltistan, akizungumzia maendeleo yanayoendelea huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, alisema:

“Mipango inayowasilishwa kwa jina la amani ya Ghaza, kwa hakika ni pazia la kuwanyang'anya silaha wapiganaji wa Kipalestina na kulinda maslahi ya utawala wa Kizayuni.”

Aliendelea kusisitiza kuwa: “Katika mazingira ambayo yamejaa dhulma, mabomu, uvamizi na ukandamizaji, kuzungumzia amani si chochote bali ni udanganyifu. Amani ya kweli itapatikana tu chini ya kivuli cha ukombozi kamili wa Palestina na kukomeshwa kwa ukaliaji.”

Msomi huyu mashuhuri wa Pakistan aliongeza kuwa: iwapo serikali ya Pakistan itaunga mkono au kushiriki katika mipango ya aina hiyo, kitendo hicho kitachukuliwa kama usaliti wa wazi dhidi ya Waislamu duniani na taifa dhalimu la Palestina, na kwamba wananchi wa Pakistan kamwe hawatakubali sera kama hizo.

Katika mwendelezo wa hotuba yake, akitahadharisha juu ya athari za maamuzi hayo, alisema:
“Historia itahukumu kwa ukali maamuzi na misimamo itakayodhoofisha mapambano ya muqawama wa Palestina. Wapakistani wamesimama pamoja na Palestina, na kamwe hawataidhinisha sera zozote zitakazonufaisha wakaliaji.”

Rais wa Jumuiya ya Imamiya Baltistan, katika sehemu nyingine ya hotuba yake, alisisitiza umuhimu wa kuadhimisha heshima na kwa fahari siku za Sha‘baniyya, hususan maadhimisho ya kuzaliwa kwa baraka ya Imam Mahdi (a.s., Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake). Pia aliwataka viongozi wa kiutendaji kuhakikisha usalama, huduma za kijamii na maandalizi muhimu katika usiku wa Barā’a na sherehe za mazazi hayo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha